Baada ya kukwama mara 2 kujadiliwa katika Bunge Muswada
wa sheria ya bima ya afya kwa wote,leo umesomwa kwa mara
ya pili Bungeni na Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu.
Akisoma Muswada huo Waziri Ummy,ameainisha marekebisho
ambayo wabunge waliyahitaji,ikiwemo kutokuwepo kwa chanzo
endelevu cha fedha kutekeleza mpango huo.
