Ujerumani yafungua mipaka yake na Luxembourg

In Kimataifa

Ujerumani na Luxembourg zimefungua mipaka yake ya barabara baada ya kuifunga kwa takribani miezi miwili. Tangu usiku wa kuamkia leo madereva wameruhusiwa kupita bila kuonesha kibali chochote. Kwa mujibu wa polisi katika mji wa Trier, maeneo 12 ya vizuizi katika eneo la mpaka yameachwa wazi. Na hakuna tena ukaguzi. Hatua za kuweka vizuizi mipakani zimezusha ukosoaji mkali katika katika maeneo mengi ya Ulaya. Kulingana na polisi ya Saarland, takribani vizuizi 35 kati ya Ujerumani na Ufaransa vilevile vimeondolewa ambapo kwa upande wa Italia vitaendelea kusalia hadi taarifa nyingne itakapo tolewa. Na taarifa ya taasisi ya afya ya Robert Koch inasema kumekuwa na ongezeko la maambukizi mapya 620 na kufanya jumla ya 173,772 na vifo vipya 57 na kufanya jumla ya 7,881.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu