Jeshi la Polisi Tanzania limesema Mwenyekiti wa Ngome ya
Vijana wa chama cha ACT Wazalendo Ndugu Abdul Nondo
alietekwa Alfajiri ya Tar moja Dec,ametelekezwa maeneo ya
fukwe za Coco, Kindondoni jijini Dar es Salaam na watu ambao
hawafahamu.
Polisi wamesema baada ya kutelekezwa katika eneo hilo, Nondo
alisimamisha bodaboda na kumwelekeza amfikishe katika ofisi
za chama chake zilizopo Magomeni,Jijini Dar es Salaam
walifika muda wa saa tano usiku.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya kufika katika ofisi hizo,
Nondo alionana na viongozi wake na kupelekwa hospitali kwa
ajili ya uchunguzi wa afya yake.
Makamu mwenyekiti wa ACT Wazalendo Isihaka Mchinjita,ni
miongoni mwa waliofika katika hospitali ya Aghakani kumjulia
hali Nondo na amezugumza baadhi ya mambo.
Kwa upande wake Kiongozi mstaafu wa chama hicho ndugu
Zitto Kabwe akizungumzia tukio hilo,amewataka watanzania
kuendelea kumwombea Nondo hali yake iwe sawa,na atapopata
nafuu ataweza kuelezea mwenyewe kile kilichotokea.



