Amjeruhi mpenzi wake kwa risasi wakiwa hotelini…

In Mahusiano


Polisi mkoani Geita inamshikilia mfanyabiashara Bw.Salum
Othman mkazi wa jijini Mwanza kwa tuhuma za kumjeruhi kwa
kumpiga risasi kwa bastola mpenzi wake Happyness Israel
wakiwa nyumba ya kulala wageni majira ya saa nne asubuhi
katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo mtaa wa Nyamalembo,kata
Mtakuja mjini Geita pamoja na kumjeruhi Meneja wa hoteli
hiyo Ndugu John Maftaa alipotaka kutoa msaada wa kumdhibiti
mtuhumiwa Salum Othman.
Taarifa hiyo imethibitishwa hapa mtaa wa mastory na Kamanda
wa Polisi Geita Mponjoli Mwabulambo huku Chanzo cha tukio
hilo kinadaiwa ni wivu wa mapenzi.


Mkurugenzi wa Hoteli Ndugu Paulo Limo yeye pia ameelezea
namna tukio lilivyotekea hotelini hapo.

Naye Kaimu Mganga mfawidhi katika hosptali ya rufaa Mkoani
Geita Dk,Shaban Massawe yeye amethibitisha kuwapokea
majeruhi wawili na pia ameelezea namna alivyowapokea
sambamba na hali zao.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Marekani yaionya vikali Russia endapo itatumia Nyuklia Kuishambulia Ukraine.

Marekani imeionya Russia kuhusu kile ilichokiita "matokeo mabaya" ikiwa itaanzisha mashambulizi ya nyuklia dhidi ya Ukraine. Mshauri wa usalama wa

Read More...

Mtoto auawa kikatili na shangazi yake

Mtoto aliyetambuliwa kwa jina la Enock Melita (4) mkazi wa kijiji cha Kiru Six kitongoji cha Ndoroboni wilayani Babati

Read More...

RUTO IMF KUONGEZA MSAMAHA WA MADENI

Rais William Ruto ametoa wito kwa mashirika ya fedha duniani kupanua msamaha wa deni la umma kwa nchi zinazoendelea

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu