Bei ya Mafuta yashuka Nchini.

In Uncategorized
LICHA ya Serikali kuongeza kodi ya Sh 40 kwa kila lita ya mafuta, bei nchini imeshuka ikilinganishwa na zile za Juni 7 mwaka huu, ambapo kwa sasa bei ya petroli kwa lita imepungua kwa Sh 37, dizeli kwa Sh 14 na mafuta ya taa kwa Sh 19 kwa lita.
Kutokana na hali hiyo, kwa Mkoa wa Dar es Salaam, mafuta ya petroli yatauzwa kwa lita Sh 2,014, mafuta ya dizeli Sh 1,874 na mafuta ya taa Sh 1,806 na kwamba katika Mkoa wa Tanga bei za rejareja za mafuta hayo zimeongezeka huku bei za jumla zikipungua.
Akitangaza bei mpya ya mafuta Dar es Salaam jana, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Titus Kaguo, kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Godwin Samwel, amesema kuwa katika mwaka uliopita wa fedha, kodi ya serikali kwenye mafuta ya petroli kwa lita ilikuwa Sh 339, mafuta ya dizeli Sh 215 na mafuta ya taa Sh 425.
Kaguo   amesema kwa sasa kodi ya mafuta ya petrol, itakuwa ni Sh 379, mafuta ya dizeli Sh 255 na mafuta ya taa Sh 465 kwa lita.
Hata hivyo, Kaguo ametoa onyo kwa wamiliki wa vituo vya mafuta ambao walihodhi kwa ajili ya kupandisha bei mafuta hayo kuanzia leo, kwamba lengo lao halijatimia, kwa kuwa bei zilizotangazwa ndizo zinazotakiwa kuanza kutumika.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu